TANGAZA NASI

header ads

Matiko aomba kura machimboni Kibaga



 Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini,Esther Matiko kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema amewaomba tena wapiga kura kumpa kura za ndio ili kwenda Bungeni kuwatetea ikiwemo kuishinikiza Serikali kutoa ufadhili wkwa wachimbaji wa dogo wadogo wa madini ikiwemo dhahabu.

Kauli hiyo aliitoa jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kibaga kunakochimbwa madini ya dhahabu ambapo aliomba kuchaguliwa na kwenda kuwasemea Bungeni.

"Mkinipa ridhaa ya kwenda bungeni nitaenda kuishinikiza Serikali ili kutekeleza sera ya madini ambayo inaitaka serikali kuwapa mikopo wachimbaji wadogo wadogo wa madini mikopo  na vifaa vya kufanyia kazi kwa lengo la kuinua kipato chenu"alisema Matiko.

Matiko aliongeza kusema kuwa endapo atapewa tena ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha miundombinu ya barabara ya Kibaga inalimwa na wasafiri wanaenda kusafiri kwa raha na kufanya biashara zao kwa raha.

Naye mgombea udiwani kata ya Kenyamanyori kupitia CHADEMA,Thomas Burure alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuwa diwani ataanza na kipaumbele cha Barabara na wapitaji kutembea kwa raha na kutumia gharama nafuu ya usafiri wa abiria na mizigo.

Mgombea huyo aliongeza kuwa wananchi wa mwamini na kumpa kura zote za ndio na wagombea wote wa Chadema akiwemo mgombea urais Tundu Lissu,mgombea ubunge,Esther Matiko ili washirikiane kuleta maendeleo ndani ya halmashauri ya Tarime.

Pia Burure alimaliza kwa kusema kuwa kabla hajawa na cheo chochote amekuwa akisaidia wananchi pale ambao wamekuwa wakionewa huku akiwatetea ikiwemo uonevu wa machimboni ambapo wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kuchimba na kusumbuliwa na watu wa chache.

Pamba Chacha alisema  kuwa Chama chake kimejipanga kushinda licha ya mgombea wake kutendewa ukatili huku akidhalilishwa kwa sababu ni mwanamke wataenda kushinda kwa nguvu ya umma na watatangazwa.

Post a Comment

0 Comments