Na Amiri Kilagalila,Njombe
Chama cha mapinduzi CCM kupitia kwa mgombea wao wa nafasi ya,Rais ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli,wameahidi kupanua bandari ya Manda wilayani Ludewa mkoani Njombe ili kurahisisha usafiri kwenye ziwa Nyasa.
Magufuli ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni zake mjini Makambako wakati akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho kwa mwaka 2015-2020 na namna watakavyotekeleza Ilani yao 2020-2025
"Tumepanga kupanua bandari ya Manda iliyopo wilaya ya Ludewa ili kurahisisha usafiri katika ziwa Nyasa kama mnavyofahamu kwenye miaka mitano iliyopita tumejenga Meli mpya tatu kwenye ziwa Nyasa kwa ghalama ya shilingi bilioni 20.4 tunataka ziwe zinatua mpaka Manda kwenye Bandari" alisema Magufuli
Vile vile amesema wako mbioni kukamilisha ujenzi wa
Chuo cha Ufundi (VETA) kinachojengwa Shaurimoyo wilayani Ludewa mkoani humo ili
kuwezesha vijana kupata mafunzo ya ufundi waweze kujiajili na kuajiliwa.
Mgombea wa Ubunge jimbo la Ludewa,Wakili Joseph
Kamonga,amesema ni shuhuda wa ujenzi wa miradi
mbali mbali ya serikali kwa kuwa alikuwa mtumishi wa serikali na anaamini Chama
cha Mapinduzi kitakwenda kukamilisha miradi inayoendelea katika jimbo hilo.
“Mimi nilikuwa mtumishi wa serikali nimeshuhudia ni
jinsi gani Rais Magufuli alivyo boresha nidhamu serikalini,ninaomba ifikapo
tarehe 28 watu wote twende tumpigie kura Dkt,John Pombe Magufuli ikiwa ni
shukrani kwa aliyotendea taifa letu”Alisema Joseph Kamonga
0 Comments