Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh Andrea Tsere amewataka vijana kujikita katika michezo hasa nyakati za jioni ili kujiepusha na vitendo viovu.
Mh Tsere aliyasema hayo katika viwanja vya michezo Ludewa mjini wakati akifungua mashindano ya mpira wamiguu yaliyoandaliwa na shirika la Padeco Pamoja na Shule ya Nicopolis Academy na kusimamiwa na shirika la Idydc ikiwa ni ishara ya kumkumbuka Prof. Ludwig kwa Mchango wake wamaendeleo kwa wilaya ya Ludewa.
Mh Tsere Alisema kuwa richa yakujihusisha namichezo lakini Vijana wanapaswa kumkumbuka tarehe 28 octoba 2020 ni siku uchanguzi mkuu hivyo vijana wanapaswa kwenda kupiga kura ili kuwachangua viongozi watakao waongoza Kwa muda wamiaka mtano ojayo.
Mratibu wa shirika la Idydc wilaya ya Ludewa na Mwenyekiti wa umoja wawaandishi wa habari mkoa wa Njombe Ndugu Nickson Mahundi amemshukuru mkuu wa wilaya hiyo kwakukubali kuyafunga mashindano hayo pia ametaka wadau mbalimbali wamaendeleo kuiga mfano wa Padeco na Nicopolis academy Kwa kuandaa mashindano hayo.
Mashindano hayo yalizihusisha timu kumi za kata ya Ludewa ambapo mshindi wa kwanza aliibuka timu ya bodaboda ambayo iliitoa kwa mikwaju ya penati tatu Kwa moja dhidi ya pamba Kali FC ambapo mshindi wa tatu alikuwa ni shule ya sekondari chief kidulile.
0 Comments