TANGAZA NASI

header ads

Wasimamizi wasaidizi Masasi watakiwa kutii sheria za uchaguzi

  

 Na Hamisi Nasri, MASASI

 WASIMAMIZI wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wametakiwa kutii sheria za uchaguzi na kanuni zake zilizowekwa na Tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) 

       Aidha,wamehimizwa kushirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika masuala ambayo wadau hao wanastahili kushirikishwa ili kuepuka sitofahamu yeyote itakayo tokea katika zoezi hilo la uchaguzi.

      Wito huo ulitolewa jana wilayani Masasi na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo,Changwa Mkwazu alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi hao wa uchaguzi ngazi ya kata kutoka Halmashauri hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa zamani wa Halmashuri hiyo mjini Masasi.

        Alisema wasaidizi hao wa uchaguzi jumla ya 68 ngazi ya kata wanapaswa kutambua kuwa wameaminiwa na kuthaminiwa na Tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) na kupewa jukumu hilo la kusimamia zoezi mzima la uchaguzi oktoba 28 hivyo lazima wafuate sharia za uchaguzi kikamilifu.

       Mkwazu alisema kuwa moja ya jukumu kubwa ambalo wanatakiwa kulifuata ni pamoja na kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na sharia zilizowekwa na Tume ya taifa ya uchaguzi.

        Alisema lakini pia katika kutekeleza majukumu yao lazima waone umuhimu wa kushirikisha vyama vya siasa pamoja na wadau wengine wa uchaguzi katika  masuala ambayo wanastahili  kushirikishwa ili kuepuka sitofahamu yeyote kutokea kwenye zoezi hilo la uchaguzi.

      “Mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mnao uwezo wa kufanya kazi hii…mambo muhimu mnayotakiwa kuzingatia ni kujiamini na kujitambua na kwamba mnapaswa kuzingatia katiba ya nchi,sharia za uchaguzi na kanuni zake,”alisema Mkwazu 

  Alieleza kuwa uchaguzi ni mchakato unaojumuhisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa kwa kuwa hatua na taratibu hizo ndio msingi wa uchaguzi kuwa wa amani na utulivu.

     Mkwazu alisema iwapo wasimamizi hao wakifanya kazi kwa ufanisi uliotukuka utasaidia kuondoa malalamiko au vurugu wakati wa mchakato wa uchaguzi.

       Alisema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo kwa wasaidizi hao wa uchaguzi ngazi ya kata ni kuwapa uwelewa wa kutosha ili katika kutekeleza zoezi hilo la uchaguzi wawe na elimu mzuri ya kufanikisha mchakato mzima wa uchaguzi.

Post a Comment

0 Comments