Na Amiri Kilagalila,Njombe
Waandishi wa habari
mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi
ya virusi vya corona (Covid-19) vinavyosababisha homa kali ya
mapafu,pindi wanapo kuwa katika majukumu yao ya kazi pamoja na kuendelea
kuhabarisha umma kuendelea kuchukua tahadhari hiyo.
Licha Taifa la
Tanzania kuwa salama dhidi ya virusi vya Corona kutokana na kuondolewa hofu ya virusi hivyo,wito
umetolewa na Bi,Eveline Kidenya afisa
afya wilaya ya Njombe kwa makundi mbalimbali likiwemo kundi la waandishi wa habari
kuendelea kuchukua tahadhari hasa pindi wanapokuwa katika mikusanyiko.
“Tuwe huru,tuishi na
kirusi hicho kama tunavyoishi na virusi wengine au Bakteria wengine,cha msingi
tusipuuzie kuendelea kuchukua tahadhari tunapokutana na wageni ambao sio wana
Njombe kwa kuwa kama Njombe tuko salama tusifikiri na watu wa maeneo mengine
wako salama”alisema Bi Eveline Kidenya
Umoja wa vyama vya
waandishi wa habari Tanzania kwaufadhili wa nchi ya sweedeni kwa kushirikiana
na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC wametoa mafunzo hayo dhidi
ya kujikinga na Corona kwa waandishi wa habari wanachama kupitia wataalamu wa
afya ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Njombe.
“Tumepata mafunzo haya
ambayo yapo katika mpango mkakati wa UTPC umoja wa vyama vya waandishi wa
habari Tanzania wakipata ufadhili kutoka ubalozi wa Sweeden kwa ajili ya
kutuwezesha waandishi wa habari kutoa habari lakini vile vile kujikinga na
maambukizi haya ya Corona”alisema Hamis Kassapa katibu wa Chama cha waandishi
wa habari mkoa wa Njombe NPC
Erasto Mgeni na Emiria
Msafiri ni baahi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika semina hiyo
wamesema wamepokea vema mafunzo hayo huku wakiadhi kuendelea kutoa elimu kwa
wananchi namna ya kundelea kuchukua tahadhari ili kujikinga na virusi hivyo.
Baadhi ya waandishi wa
habari wa mkoa wa Njombe,wawakilishi kutoka vyombo mbambali vya habari nchini
Tanzania wakati wakikumbushwa mambo mbali mbali juu ya magonjwa ya mlipuko
hususani mambukizi ya virusi vya Corona katika semina iliyofanyika hii leo
ukumbi wa Dosmeza mjini Njombe.
Bi,Eveline Kidenya
afisa afya wilaya ya Njombe wakati akitoa maelekezo juu ya magonjwa ya mlipuko
na virusi vya Corona.
Katibu wa Chama cha
waandishi wa habari mkoa wa Njombe NPC Ndugu Hamis Hassan Kasapa akizungumza
jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa semina ya siku moja juu ya
kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya milipuko hususani Corona.
0 Comments