Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu,Sera,Ajira,Vijana na Wazee, Jenista Mhagama amefanya ziara katika
ofisi za mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mkoani Njombe na kuonyesha
kutoridhishwa na utendaji wa kazi ndani ya ofisi hiyo na kutoa agizo kwa meneja
wa NSSF mkoa huo kuwa na mkakati mahususi utakaowezesha mfuko huo kuongeza kasi
ya ukusanyaji wa michango.
“Na mimi
nimeshatangaza mgogoro na mameneja ambao hawafikishi malengo ambayo sisi
tunafikiri wanao uwezo wa kuyafikisha,bodi na mkurugenzi waondoeni hao tutafute
meneja mwingine”alisema Jenista
Ni Mheshimiwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira, Vijana na Wazee, Jenister Mhagama
akitoa msistizo kwa Mameneja wanaotumikia ofisi za mifuko ya taifa ya hifadhi
ya jamii nchini kuwajibika ipasavyo katika utendaji wao ili kutimiza lengo la
serikali wakati alipotembelea ofisi za NSSF mkoa wa Njombe na kuzungumza na
wafanyakazi wa mfuko huo na hapa anasema…
“Jambo jingine ambalo
nimejifunza hapa hamna mikakati,ipo miradi ya kimkakati ambayo inaendelea
kwenye mkoa huu bado hamjaifikia lakini zipo sekta zisizorasmi bado
hamjazifikia”aliongeza Jenista
“wote ambao manataka kuwafikia
wapo ndani ya wilaya ni lazima mjenge mahusiano vunjeni hizo kuta”alisema Ruth
Msafiri mkuu wa wilaya ya Njombe
Awali Meneja wa NSSF
mkoa wa Njombe, Mrisho Mwisimba akabainisha miongoni mwa changamoto
zinazowakabili katika mwaka wa fedha uliopita.
“Uwepo wa wahazini
wadaiwa wa michango umepelekea kushindwa kufika lengo la ukusanyanyi pamoja na
kuchelewa kulipa wanachama kwa wakati”alisema Mrisho Mwisimba Meneja wa NSSF
mkoa wa Njombe
0 Comments