Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mjasiriamali Ruben Mtitu maarufu Mzee Kisangani Aliye Buni
kiwanda cha kufua vyuma kutokana na madini ya mawe ya chuma na makaa ya
mawe mkoani Njombe amemshangaza Waziri wa Viwanda na Biashara, Inocent
Bashungwa Baada ya kuanzisha kiwanda ambacho amesema
kitakuwa msaada kwa taifa katika
kulahisisha kupatikana kwa mali ghafi mbalimbali.
Waziri Inocent Bashungwa amefika katika kijiji cha
Mkiu, Kata ya Madope wilayani Ludewa akiwa ameongozana na ujumbe wa viongozi wa
Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Madini kuona kiwanda cha
mbunifu huyo, kikiwemo chanzo cha kuzalisha umeme wa nishati ya maji.
“Lakini teknolojia ambayo
mnaiihitaji ili jiwe ili itoe Chuma na sisi tuna taasisi,katibu mkuu Prof,Shemdoe
tumekuja nae tuangalie changamoto mnazokabiliwa nazo hizo taasisi zifike hapa
tuangalie ni namna gani mnaweza kuzalisha na mpate hela”alisema Bashungwa
Kutokana na ujumbe wa viongozi wa Wizara ya viwanda kufika katika eneo ambalo
kiwanda cha kutengeneza zana mbalimbali
kwa kutumia Madini ya mawe ya chuma
Mzee Rubeni Mtitu amezungumzia ujio wa waziri viwanda na Biashara Njombe
“Tunashukuru kwa
ushirikiano pamoja na sisi” alisema Mzee Mtitu
Hata hivyo waziri Bashungwa kwa kushirikiana na Wizara ya Madini pamoja na
Wizara ya Nishati ameahidi kuwa wataendelea kumuunga mkono mjasiriamali huyo
ili uzalishaji wa bidhaa muhimu zitonakazo na chuma ziweze kuzalishwa kwa ingi hapa nchini.
Katika kukamilisha ziara yake mkoani Njombe bashungwa ametembelea kiwanda cha
kusindika Parachichi cha Olivado kilichopo wilayani Wanging'ombe na kuwataka
wananchi kuendelea kulima zao la Parachichi kwa kuwa serikali inaandaa miundo
mbinu bora ya upatikanaji wa soko.
0 Comments