Na Amiri Kilagalila,Njombe
Waziri wa ujenzi Uchukuzi na mawasiliano Eng,Isack
Kamwelwe amemuagiza mkandarasi anayejenga mradi wa barabara kipande cha Kilomita
50 kutoka Lusitu kwenda Mawengi ambayo ni sehemu ya Itoni-Ludewa-Manda wilayani
Ludewa Mkoani Njombe kwa kiwango cha zege,kuweka mipango vizuri ya ujenzi ili
kuhakikisha bara bara hiyo inakamilika kwa kuwa mradi huo umeanza muda mrefu na
kushindwa kukamilika mpaka sasa.
Waziri Kamwelwe ametoa agizo hilo alipotembelea na kukagua maendeleo ya barabara hiyo mkoani
Njombe na kushindwa kuridhika kutokana na kuchukuwa muda mrefu huku ikiwa bado
haijakamilika.
“Kazi hii ilianza mwezi Disemba mwaka 2016,kwa hiyo 2017
imeisha, 18 imeisha, 19 imeisha na tuko sasa 20 mwezi wa nane.Mkandarasi huyu
anaonekana ni mgeni pamoja na kwamba wakati wa manunuzi alionekana ana uwezo
mkubwa,kazi anayofanya ni nzuri lakini naona alishindwa kufanya mipango”alisema
Waziri Kamwelwe
Aidha Waziri Kamwelwe amesema mkandarasi anayejenga
bara bara hiyo ameshindwa pia kwenda na wakati kutokana na kuwa na mitambo
michache hivyo hatarajii kuona anapewa nyongeza ya muda.
“Mitambo aliyoleta imekuwa ni michache hasa ya
kubeba udongo ndio maana amechukuwa muda mrefu,mradi huu ulikuwa na wa miezi 28
wakamuongezea ikafika miezi 46 ambayo inaisha mwezi wa 10 mwaka huu,mimi
sitarajii wampe tena nyongeza ya muda na kama mhandisi mshauri atataka
ziongezeka fedha za kumlipa basi serikali haita toa hilo ndio agizo
langu,mkandarasi kwasababu yeye ndio aliyechelewesha tutakuwa tunamega hela
yake halafu tunalipa mshahara wa msimamizi” aliongeza Kamwelwe
Vile vile ameagiza wakala wa barabara Tanzania
TANROADS kupeleka wataalam waweze kuongeza bidii kusimamia kazi hiyo kwa kuwa
bara bara hiyo itatumika kubeba mzigo mkubwa pindi itakapoanza zoezi la
uchimbaji wa madini ya Chuma na makaa yam awe hivyo ni lazima asimamiwe ili
kazi hiyo iweze kukamilika mapema mwezi Octoba.
Aidha kwa upande wake meneja wa TANROADS mkoa wa
Njombe mhandisi Yusuph Mazana,amesema mradi huo uliopo chini ya mkandarasi
Cheon Kwang Engenginearing & Construction Copamany ya Korea
Kusini,unaotarajia kujengwa kwa ghalama ya shilingi Bilioni 179.17 za fedha za
serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100%, mpaka sasa
umefikia asilimia 45.35%
“Utekelezaji wa mradi huu ambao unatakiwa ukamilike
tarehe 30 Octoba,2020 mpaka sasa umefikia asilimia 45.35, na mpaka sasa
mikakati ya kupunguza kuchelewa kwa kazi,mkandarasi ameleta wataalam makini
sasa hivi,mkandarasi ameweza kuleta vifaa vyote vinavyotakiwa na ameongeza kasi
ya ujenzi kwa kufanya kazi kwa muda mrefu”alisema Mazana
0 Comments