TANGAZA NASI

header ads

Clouds FM, CloudsTV zafungiwa siku saba

 


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Clouds FM na CloudsTV kwa siku saba kuanzia kesho Agosti 28, mpaka Septemba 3, 2020 kwa kukiuka kanuni za utangazaji na miongozo ya utangazaji kipindi cha uchaguzi.

Mtendaji Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, amesema pia Clouds itumie muda wa masaa yote ya leo kuomba radhi kwa makosa hayo.

Kwa mujibu wa TCRA, Clouds FM na Clouds TV kupitia vipindi vya Power Breakfast na Clouds 360 walirusha takwimu za wagombea waliopita bila kupingwa bila kuthibitishwa.

Post a Comment

0 Comments