TAKUKURU wamhoji Kibajaji
Charles James
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Mkoa wa Dodoma imekiri kumhoji Mbunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma,
Livingston Lusinde 'Kibajaji' kwa tuhuma za kuwakusanya wajumbe wa Chama cha
Mapinduzi wilaya ya Chamwino na kuwahonga.
Akizungumza na Michuzi Blog, Kamanda wa Takukuru
Mkoa wa Dodoma, Sosthnes Kibwengo amekiri kumhoji kwa masaa mawili Mbunge huyo
jana na kumuachia na kwamba uchunguzi zaidi juu ya tuhuma hizo bado unaendelea.
Kibwengo anasema Ofisi yao ilipata taarifa za Kibajaji kuwakusanya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama wa wilaya na wale wa Umoja wa
Wanawake Tanzania UWT wilaya ya Chamwino kwa lengo la kuwapatia fedha kwa ajili
ya ushawishi ili wamsaidie kwenye kampeni zake za Ubunge.
" Hakuwekwa ndani ila tulimhoji katika Ofisi
zetu za Takukuru Wilaya Chamwino kwa masaa mawili au matatu hivi, na taarifa
tulizopata ni kwamba anakusanya watu na kuwahonga hatukupata ushahidi wa yeye
kuhonga lakini uchunguzi wa hilo jambo bado unaendelea," Amesema Kibwengo.
Usiku wa kuamkia leo kulizuka taarifa za kushikiliwa
kwa Mbunge huyo sambamba na baadhi ya wajumbe na wanachama wa CCM.
(VIA:Michuzi TV)
0 Comments