TANGAZA NASI

header ads

Rais Magufuli asema shule za msingi na sekondari zipo mbioni kufunguliwa

 One year to go for Tanzania′s President Magufuli and the reviews ...
Rais wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema atafungua shule za msingi na sekondari hivi karibuni, kama ataridhishwa na kasi ya upunguaji wa maambukizi ya virusi vya Corona


Magufuli aliyasema hayo jana Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jijini Dodoma.

Amesema, maambukizi ya corona yamekuwa yakipungua siku hadi siku huku akiendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari  ya ugonjwa huo.
Hali kadhalika Rais Magufuli amefurahishwa na washiriki wa mkutano huo walioujaza uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutokuvaa barakoa huku akionyesha kushangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuvaa barakoa akiwa ndani ya Bunge. 
“Corona imekwisha ndiyo maana hata mabarakoa hakuna, hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndiyo maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kwenye kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu."alimesema.

Post a Comment

0 Comments