TANGAZA NASI

header ads

Rais Dkt. John Magufuli,atangaza mfumo wa ukusanyaji na ulipaji wa madeni ya watumishi

 
Serikali inaandaa mfumo wa kielektroniki, utakaotumika katika kukusanya na kulipa madeni yote ya watumishi wa umma, ili kuondokana na tatizo la udanganyifu uonakosababisha kuwepo kwa madeni hewa.
Rais Dkt. John Magufuli, alitangaza mpango huo wa serikali  jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), unaoambatana na uchaguzi mkuu wa viongozi wa chama hicho, na kusisitiza serikali inaendelea kulipa madeni ya watumishi wake wakiwemo walimu, lakini ni mara  baada ya kuhakiki madeni hayo.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli akachukua wasaa huo kuwahimiza watanzania kwa mara nyingine tena, kuacha kupokea misaada ya barakoa wasizozijua zinatoka wapi, huku akiwakumbusha viongozi wa ngazi mbalimbali wajibu wao wa kuwalinda wananchi.

Post a Comment

0 Comments