TANGAZA NASI

header ads

Makonda ataoa maagizo Dar es salaam

 Tanzania's Makonda To Arrest All Gays Within 7 Days

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuelekeza Kamanda wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha wanawashughulikia ipasavyo baadhi ya vijana walioanza tabia ya kupora na kuiba Mali za Watu jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya Watu.


Mhe. Makonda ametoa agizo hilo wakati wa Ziara ya ukaguzi miradi ya maendeleo Wilaya ya Temeke iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Majengo ya Madarasa 124, Matundu 124 ya Vyoo na Madawati 7,179 kwenye Shule ya Sekondari Mbagala na Shule nyingine 16 Wilayani humo jambo linalokwenda kusaidia zaidi ya Wanafunzi 5,000 waliofaulu na kukosa nafasi kupata uhakika wa kuendelea na masomo.


hali lkahalika  kiongozi huyo ametembelea Ujenzi wa kituo cha Afya Buza na Hospital ya Yombo Vituka yenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 2,000 kwa Siku ambapo amesema kuongezeka kwa Zahanati, Vituo vya Afya na Hospital vinakwenda kurahisisha upatikanaji wa Huduma za Afya kwa wananchi.


Pamoja na hayo RC Makonda amesema ifikapo Juni 20 ataanza Ziara ya Siku 10 na Kamati ya Siasa ya Mkoa kwenye kila jimbo kwa lengo la kukabidhi miradi iliyokamilika ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Vitendo.


Katika Ziara hiyo RC Makonda  ametembelea Ujenzi Mitaro yenye urefu wa Km 9 Wilayani humo ikiwemo mtaro mkubwa kabisa unaojengwa eneo la Serengeti kuelekea Shule ya Sekondari Kibasila na Maradi na Mradi wa uwezeshaji wa vijana kupitia 10% ya mikopo inayotolewa kwenye halmashauri ambapo ameipongeza Manispaa hiyo kwa namna inasimamia miradi ya maendele
o

Post a Comment

0 Comments