China
imesema itafuta mikopo isiyokuwa na faida iliyokuwa kama mzigo kwa
mataifa mbalimbali ya Afrika wakati huu ambapo nchi za bara la Afrika linalopoendelea
kukabiliana na janga la Corona.
Akizungumza
na viongozi wa nchi hizo kupitia mfumo wa Video, rais Jinping pia
amezitaka taasisi za fedha za China kuwa na mazungumzo ya kirafiki na
nchi za Afrika kuona namna watakavyolipa madeni yao.
Aidha,
katika hatua nyingine, amesema nchi yake itasimama na bara la Afrika
katika vita dhidi ya Corona na kufadhili ujenzi wa makao makuu ya
kudhibiti magonjwa barani Afrika jijini Addis Ababa.
Bara la Afrika kwa sasa lina maambukizi zaidi ya Laki Mbili na vifo zaidi ya Elfu saba kutokana na janga la Corona.
0 Comments