Mkurugenzi mkuu wa
NIMR, Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa wanapendekeza aina tatu za mchanganyiko
wa mimea tiba kutengeneza joto tiba au mvuke kwaajili ya kujifukiza kuondokana
na virusi vya magonjwa mbalimbali ikiwemo hili la virusi vya Corona.
Aliutaja aina ya
kwanza ya mchanganyiko wa mimea ambayo wananchi wanaweza kuutumia ni
mchanganyiko wa majani ya mkaratusi, majani ya kivumbasi au kashwagala na
majani ya mchaichai.
Aina ya pili ni
mchanganyiko wa majani ya mchaichai, karafuu, tangawizi iliopondwapondwa na
majani ya mlimao. Aliutaja aina ya tatu ni kuwa ni mchanganyiko wa majani ya
mwarobaini, majani ya mpera, mchaichai na majani ya mlimao.
Kwa mujibu wake, tiba
joto hiyo au mvuke ni muhimu kwani inasaidia kuongeza kinga ya mwili, kufungua
njia ya hewa na kukirarua kirusi cha corona kama bado kiko kwenye njia ya hewa
na hakijaingia kwenye mapafu.
Alisema tiba ya
kujifukiza haisaidii kama tayari kirusi cha corona kimeshaingia kwenye mapafu,
hivyo mgonjwa anatakiwa kupewa matibabu mengine ikiwemo antibiotic.
Prof.Mgaya alishauri
mvuke huo unahitaji Joto la nyuzi 50-70. Anasema “Joto la mvuke linatakiwa liwe
kati ya nyuzi 50 hadi 70, likizidi linaweza kuumiza njia ya hewa, mtu anatakiwa
avute mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni, watu wazima wavute kwa dakika
nane hadi kumi na watoto kuanzia umri wa miaka saba wavute kwa dakika mbili
hadi nne, watoto chini ya miaka saba hawaruhusiwi kutumia tiba hii,” alisema
Profesa Mgaya.
Kwa kuwa mvuke una
kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni, alisema watu wenye matatizo ya kupumua
hawapaswi kutumia tiba hiyo kwani wanaweza kupoteza maisha, pia wanaotumia
wasijifukize wakati sufuria iko kwenye jiko la mkaa bali iwekwe chini au mahali
pengine kwa kuwa mkaa hutoa hewa yenye sumu hatari kwa binadamu.
Kuhusu maandalizi ya
dawa hiyo, Profesa Mgaya alisema hatua ya kwanza ni kuchemsha maji ya lita tano
au kumi hadi yachemke, kisha yawekwe majani na kuyafunika na kuyachemsha kwa
dakika tano tu.
Alisema dawa
ikichemshwa kwa zaidi ya dakika tano inakuwa imepikwa na haifai kwa tiba kwa
sababu virutubisho muhimu vinakuwa vimepotea kwa njia ya mvuke.
Alisema wakati wa
kujifukiza mtu anaweza kujifunika kwa blanketi au shuka au taulo zito ili mvuke
usipotee, na baada ya kujifukiza muhusika asipewe maji baridi ya kunywa kwani
ataharibu tiba bali apewe glasi ya maji ya moto au chai.
Kuhusu kipimo cha
dawa hizo, alitoa kipimo kwa mchanganyiko wa kwanza tu ambapo mtu anatakiwa
atumie gramu 50 za majani ya mkaratusi na gramu 50 za kivumbasi na gramu 20 za
mchaichai.
(Fullshangwe)
0 Comments