Na Clief Mlelwa,Makambako
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Magongo uliopo kata ya
Makambako mkoani Njombe wameamua kuendeleza maeneo yao kwa kujenga nyumba licha
ya serikali kuzuia wasiendeleze kwa madai ya kwamba eneo hilo ni la hifadhi ya
msitu wa halmashauri.
Wananchi hao wamesema kuwa wameamua kujenga nyumba
hizo baada ya kukaa takribani miaka 30 bila kupatiwa suruhisho ya kuendeleza
maeneo hayo licha ya kuwa ni maeneo yao halali.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa kitendo cha
serikali kusema wasiendeleze maeneo hayo kimepelekea wapate adha kubwa hasa
kiuchumi.
Nae mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa magongo
NICODEM MAKINDA amesema kitendo cha wananchi kuamua kuendeleza maeneo yao ni
ishara tosha kwamba wamechoka kusubiri maamuzi ya mwisho kutoka kwenye mamlaka
husika hasa serikali.
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako
PAULO MALALA amesema kuwa hana taarifa ya wananchi hao kuendeleza maeneo hayo
na kueleza kuwa endapo yanaendelezwa basi watakuwa wamevamia kwa kuwa eneo hilo
halijaruhusiwa kuendelezwa kwa shughuli yoyote.
0 Comments