Na Joctan Myefu,Njombe
Watu wanaopindukia 162 kutoka halmashauri kumi na
tano wakiwemo waratibu wa ukimwi wamekutana
mkoani Njombe kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi kupitia mradi
wa hebu tuyajenge ili kufikia asilimia tisini na tano tatu hapa
nchini.
Mradi huo unaotekelezwa na baraza la taifa la watu
wanaoishi na mambukizi ya virusi vya ukimwi Nacopha kwa ufadhili wa serikali ya
watu wa Marekani USAID ambapo katika kanda ya Mbeya umefanyika mkoani Njombe
ukianza na washiriki kutoka halmashauri tisa.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo watu
wanaoishi na virusi vya ukimwi akiwemo daud kisunga,john msamvu na joyce
samson wamesema hali ya unanyanyapaa wa
watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi imepungua kutokana na
kuongezeka kwa uelewa kuhusu ukimwi na virusi vya ukimwi huku changamoto
ikibaki ndani ya familia.
Wakizungumzia mradi huo washiriki hao wamesema
utasaidia kuwarejesha watu walioacha kutumia dawa na ambao wanakwepa kupima
virusi vya ukimwi.
Awali akifungua mafunzo hayo kaimu mganga mkuu mkoa
wa Njombe Dr. David Ntahindwa kwa niaba ya mganga mkuu amesema ujuzi
wanaopatiwa mawakili tiba ama waviu katika mafunzo hayo utumike kama muongozo
wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya jamii.
Mradi huo unatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miaka
mitano ambapo katika kanda ya mbeya umehusisha washiriki kutoka mikoa ya mbeya,
Njombe na iringa.
0 Comments