Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi ametoa sababu za Tanzania kutoshiriki kwenye mikutano ya kikanda ukiwemo mkutano wa Korido ya Kaskazini wa Jumuiya ya Afika Mashariki unaohusisha nchi nne pamoja na mkutano wa SACU uliotishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Profesa Kabudi alitoa ufafanuzi huo jana Mei 13,2020 Bungeni Mjini Dodoma
Profesa
Kabudi alianza kwa kuelezea mkutano uliohusisha nchi nne ambazo
zinaunda Korido ya Kaskazini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo
alisisitiza mkutano huo haukuwa unaihusu Tanzania ingawa ilikuwa na
taarifa za kufanyika kwake.
"Mkutano
ambao umefanyika ni wa Korido ya Kaskazini na walitutaarifu na tulijua,
kwanini walitutaarifu lakini kwanini tuhudhurie mkutano wa Korido ya
kaskazini? Ni wa kwao , ule haukuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
"Na
sitaki kurudia aliyoyasema Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2012, hayo
yamepita tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya hii ya
Afrika Mashariki. Wana yao na sisi tusiwe sehemu ya hayo, ndwele si sifa
lakini Tanzania haijawahi kuacha kusimamia maslahi yake pamoja na udogo
wa nchi hii kiuchumi.
"Nchi
hii imefanya mambo makubwa sana kwa hiyo nataka kuwahakikishia mkutano
ule wa zile nchi nne ulikuwa ni mkutano wa majadiliano wa Korido ya
kaskanini,lakini sisi na Rwanda tumekuwa na centre Corido , ndio maana
sisi na Burundi hatukwenda, kwasababu Burundi ni Centre Corido.Kwanza
utafanyikaje bila sisi kualikwa.Kwanza nilitaka hilo lieleweke na watu
wasikuze,"alisema Profesa Kabudi wakati anatoa ufafanuzi.
Kuhusu
mkutano ulioitishwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Profesa
Kabudi alisema kuwa Rais huyo hakuitisha mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),kwani mikutano ya SADC inaitishwa na
Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Mwenyekiti( Mwenyekiti
wa Sasa wa SADC ni Rais Wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli)
Alisema
kuwa mkutano uliotishwa na Rais Ramaphosa ulikuwa ni mkutano wa nchi
ambazo ni majirani wa Afrika Kusini(SACU)ambao wengi wao wako SACU
ukiondoa Zimbabwe ingawa inapakana na Afrika kusini, Msumbuji na Angola
na ndio maana nchi nane hazikuhudhuria.
Profesa
Kabudi alizitaja nchi ambazo hazikuhudhuria mkutano huo wa SACU ni
Tanzania, Zambia, Malawi,Madagasca, Mauritius, Comoro na DRC
0 Comments