Wizara ya afya nchini Kenya imesema kuwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini Kenya yamefikia 758 baada ya watu 21 zaidi kuthibitishwa kuwa na virusi vya Corona baada ya sampuli 1486 kupimwa katika muda wa saa 24 zilizopita.
Aidha idadi ya waliofariki imeongezeka na kufikia 42 baada ya watu wawili zaidi kufariki hapa Nairobi.
Vilevile idadi ya waliopona imefikia 284 baada ya watu wengine 3 kupona na kuondoka hospitalini.
0 Comments