TANGAZA NASI

header ads

Zuchu avaa uungwana,ataja wimbo alioandikiwa na bosi wake



Akizungumza na kipindi cha The Switch cha Wasafi FM amesema wimbo huo ni Mauzauza ambao amemshirikisha Mama yake mzazi, Khadija Kopa.

“Ni wimbo ambao ulirekodiwa usiku kabla ya kuachiwa kwa EP yangu, uliandikwa na Mbosso, Boss (Diamond) pamoja na Mama,” amesema.

EP hiyo inayokwenda kwa jina la I Am Zuchu alitoka rasmi Aprili 12, 2020. Nyimbo nyingine ni kama Hakuna kulala, Nisamehe, Kwaru, Wana na Raha.y

Ikumbukwe Februari mwaka huu msanii mwengine wa WCB, Rayvanny aliachia EP yake inayokwenda kwa jina la Flowers ikiwa na nyimbo nane.

Zuchu ameungana na wasanii wengine wa Bongo Fleva waliotoa EP kwa kipindi cha hivi karibuni. Wasanii hao ni kama Mimi Mars, Harmonize, Barnaba, Lulu Diva na wengineo.

@bongoswaggz.com

Post a Comment

0 Comments