TANGAZA NASI

header ads

Watendaji 7 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa kutumia mashine za POS


Na Amiri kilagalila,Njombe

Takukuru mkoa wa Njombe imewafikisha mahakamani wilaya ya Makete maafisa 7 watendaji  wa vijiji kwa wizi wa fedha Tshs.99,321,466/- za halmashauri ya wilaya ya Makete,ambazo zilikuwa ni makusanyo ya mapato ya halmashauri kwa kutumia mashine za POS (Point of Sale electronic Machine)

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Njombe Bi.Domina Mukama, amesema amesema kesi zilizofunguliwa mahakamani za maafisa watendaji hao wa vijiji ni.

1.CC.12/2020 Jamhuri dhidi ya Chrispin Raphael Ngonela mtendaji wa kijiji cha Matamba wilayani Makete anayeshtakiwa kwa kosa la wizi wa jumla Tshs. 24,356,656/=

2.CC.13/2020 Jamhuri dhidi ya Exavery Pius Mwabena mtendaji wa kijiji cha Ikungula wilayani Makete anayeshtakiwa kwa kosa la wizi wa jumla ya Tshs 3,038,022/=

3.CC.14/2020 jamhuri dhidi ya Elia Mose Nguvila mtendaji wa kijiji cha Ndapo wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa jumla ya Tshs 7,968,060/=

4.CC.15/2020 jamhuri dhidi ya Benson Anyingisye Mbwilo mtendaji wa kijiji cha Ludodolelo wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa jumla ya Tshs 16,220,098/=

5.CC.16/2020 jamhuri dhidi ya Salim saleh Salim mtendaji wa kijiji cha Kisinga wilayani Makete anayetuhumiwa  kwa kosa la wizi wa jumla ya Tshs 28,212,970/=

6.CC.17/2020 jamhuri dhidi ya Ebson Issa Mahenge mtendaji wa kijiji cha Mbalache wilayani Makete anayetuhumiwa kwa wizi wa jumla ya Tshs 14,350,160/=

7.CC.18/2020 jamhuri dhidi ya Victor Frank Mapunda mtendaji wa kijiji cha Ilindwe wilayani Makete anayetuhumiwa kwa kosa la wizi wa jumla Tshs 5,175,500/=

Na kufanya jumla ya kiasi cha fedha kilichoibwa na watumishi hao kupitia mashine za POS kuwa Tshs. 99,321,466/=.

Mukama amesema katika watuhumiwa hao jumla ya watuhumiwa wanne ambao mashtaka yao yanazidi milioni 10 wamekosa dhamana kwa kushidwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama hiyo ikiwa ni pamoja na kuwe nusu ya fedha ambazo zinatuhumiwa kuibwa na watuhumiwa hao ikiwa ni matakwa ya kisheria chini ya kifungu cha 148 (5) (e) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya Jinai Sura ya 20 marejeo ya mwaka 2002.

Aidha Mukama ametoa wito kwa watendaji wa vijiji,kata na watu walioaminiwa na serikali kukusanya mapato ya halmashauri na kuwasilisha kwa usahihi fedha zote katika akaunti za halmashauri .

Vile vile Takukuru mkoa wa Njombe inawataka wananchi na watumishi wote wa umma kuwa wazalendo na kuungana na serikali katika vita dhidi ya Rushwa ili kujenga na kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments