Mgonjwa anayetokana na virusi vya Corona (Covid-19),ametoroka karantini jijini Dar es Salaam,Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amethibitisha kushikiliwa basi za kampuni ya Luwinzo mjini Makambako zilizotumiwa na mgojwa huyo na kuendelea na ukaguzi.
Msafiri amesema serikali inafuatilia kwa karibu chombo cha usafiri kilichotumiwa na mgonjwa huyo aliyetoroka karantini.
“Hizo taarifa ni za kweli lakini bado wanafanyia kazi hawajanipa taarifa ni Luwinzo ipi kwasababu zipo Luwinzo tatu,kwa hiyo wameisha kamata Luwinzo ya Kwanza wanasubiri zingine na zote baadaye watakagua watathibitisha ni ipi na itabaki hiyo hiyo moja”alisema Ruth Msafiri
Aidha mkuu huyo wa wilaya ameto wito kwa wananchi kuendelea kujikinga na virusi hivyo vya Corona.
“Wito wangu ni kwamba lazima tukubali Corona ipo na dawa ya kwanza unikinge,nikukinge yaani tukingane na inapotokea umethibitika utulie na utapata huduma zote sasa unapokimbia unaleta taharuki na unaleta shida kwasababu unaleta ugonjwa kutoka eneo moja kwenda eneo lingine”amesema Ruth Msafiri
Vile vile amesema serikali haitaruhusu watu kukusanyika wala kukimbilia katika maeneo yaliyowekwa kwa ajli ya washtukiwa na badala yake wananchi waache vyombo vya tiba na vya usalama kusimamia swala hilo.
0 Comments