Mjumbe wa kamati kuu Chadema, Mhe,Patrick Ole Sosopi kwa mara nyingine tena baada ya kuguswa na hali mbaya ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea tarehe 20.03.2020 katika kitongoji cha Mbingama.
Ole Sosopi alifika Jimbo la Isimani, tarafa ya Pawaga, kata ya Mlenge, kijiji cha Isele, kitongoji cha Mbingama hapo jana kwa awamu ya pili, ikumbukwe kwamba alitembelea wahanga Kwa mara ya kwanza tarehe 03.04.2020 na kutoa msaada wa chakula, unga sembe kilo 200.
Jana amefika tena kuwaona wahanga na kutoa msaada Wa Chakula, unga wa sembe musu tani kwa Wahanga wa Mafuriko pamoja na Loba Mbili za Nguo, ikiwa ni kitihada za kuwasaidia wananchi hao walio atharikika sana na mafuriko na kupotelewa na kila kitu na kukosa mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Tar 20.03.2020 kitongoji cha Mbingama kilipata mafuriko makubwa na kupelekea Wananchi zaidi ya 800 na zaidi ya Kaya 201 kupoteza makazi, mavazi, chakula na mali mbalimbali.
Mhe Ole Sosopi akiwa ni sehemu ya wanafamilia wajimbo la Isimani, na kwa kutambua kwamba wahanga wanauhitaji wa mahitaji mengi sana yeye binafsi alimua kutafuta namna ya kwenda kuwafariji, kwa kushirikiana Viongozi wa chama, marafiki zake, wadau mbalimbali ili waweze kuchagia kutafuta chakula kama hitaji kubwa zaidi kwa wahanga,
Aidha amejionea watu wakiwa wanaishi kwenye mahema na mazingira magumu na Hii bado inaonesha kuna uhitaji mkubwa sana, wa chakula, Mabati kwa ajili ya kuezeka nyumba zao punde ujenzi utakapoanza.
Mhe. Ole Sosopi amendelea kutoa wito kwa marafiki zake na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi wanao wiwa au wanaotamani kutoa michango ya vitu kwa Hali na Mali waweze kutumia utaratibu kama huu wa kuwasiliana naye na kuweza kuendelea kukusanya michango mbalimbali au wanaoweza kwenda basi wafike na kutoa misaada kwa Wahanga.
Hata hivyo ametumia fursa hii kuwashukuru marafiki zake, wadau na Viongozi mbalimbali kwa kumuunga mkono kwa mchango wa unga kilo 550kg ambazo amekabidhi jana kwa Diwani wa Kata ya Mlenge, Mwenyekiti wa Kijiji Isele na Mwenyekiti Kitongoji Mbingama na mbele ya wahanga wenyewe,Kwa awamu ya Kwanza kilo 200kg na Awamu ya pili jana kilo 550kg, jumla ya kilo za Unga wa Sembe aliotoa msaada umefikia kilo 750kg.
Ole Sosopi alimbatana na Mhe. Jackson Mnyawami Katibu Kanda ya Serengeti, Mhe. Frank John Nyalusi Diwani Manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa Madiwani Chadema, Mkoa wa Iringa na Mhe. Hamida Tanda, Katibu wa Chadema, Iringa(W), Richard Ligoha Mwenyekiti wa Bavicha Iringa(w) na Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Isimani.
0 Comments