TANGAZA NASI

header ads

Njombe:Kijana anusurika kuuawa kwa tuhuma za kuiba gunia za mkaa



Na Amiri kilagalila,Njombe

Mtu mmoja anaefahamika kwa jina la Issa Setti maarufu Mngoni ambaye ni dereva bodaboda kituo cha Lutilage mjini Njombe amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kali wa mtaa wa Idundilanga akituhumiwa  kuiba gunia mbili za mkaa.

Wakizungumza kwa hisia kali wakazi wa mtaa huo wenye mikasa mingi ya wizi na uporaji akiwemo Joseph Kasiani na Grace Michael wamesema kijana huyo amekuwa na tabia ya wizi na udokozi wa kupindukia kwa kipindi kirefu na kutupiwa lawama na watu wengi.

Wakazi hao wanasema kijana huyo ambaye ni dereva bodaboda amekuwa akifanya kazi ya bodaboda nyakati za mchana na usiku kufanya matukio ya kialifu na kusababisha hasara kwa watu wengi hatua ambayo inawafanya kuona ulazima wa kumfukuza mtaani kwao kijana huyo anaetoka mkoani Ruvuma.

“Yaani waizi ni kero hii nichangamoto kubwa kwetu sisi unaweza ukakaa hapa kijiweni lakini unawaza huko nyumbani kuibiwa,lakini hata hivyo ni kweli yeye amekiri gunia mbili hizo amezibeba baada ya sisi kumhoji”walisema wananchi waliomuweka kati kati mtuhumiwa huyo

Akihojiwa na wananchi kuhusu kuhusika na matukio mbali mbali ya wizi likiwemo la wizi wa mkaa kijana huyo anaetuhumiwa kwa wizi amekiri kuhusika na vitendo vya wizi na kuahidi kubadilika endapo atasamehewa.

“Kwa kweli juzi tu nilipitiwa”alisema Issa Setti

Kwa upande wake Albeti Danda mfanyabiashara wa mkaa anasema amekuwa akimtafuta mwizi wake kwa kipindi kirefu kwani ameibiwa zaidi ya gunia 100 tangu aanze biashara hiyo huku mjumbe wa serikali ya mtaa wa Idundilanga ambaye hakutaka kuwekwa wazi jina lake akisema naye alishawahi kuibiwa kreti 5 na kijana huyo hivyo apelekwe katika vyombo vya sheria ili hatua zichukuliwe.

“Mimi mwenyewe huyu kwangu aliiba makreti yangu matupu ya bia matano nikamtafuta akanikimbia na imepita miezi miwili tu leo amekamatwa tena”alisema mjumbe wa serikali ya mtaa

Mara baada ya kuadhibiwa na wananchi wa  mtaa huo kijana huyo amefikishwa polisi


Post a Comment

0 Comments