TANGAZA NASI

header ads

Watanzania watakiwa kutumia siasa kwa maendeleo



Watanzania wametakiwa kuitumia siasa kama kichocheo cha kuleta maendeleo nchini na kuepuka mikanganyiko ya kisiasa ambayo hutokea katika mataifa mbalimbali duniani ambayo huchochea kuharibu amani.

Rais wa shirika La elimu ya amani Wilsoni Munguza ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabri ambapo amesema siasa ikitumiwa vizuri husaidia kuchochea kuleta maendeleo chanya ikiwemo ya kiuchumi, kiutamaduni na kijamii, ambapo watu wanapaswa kutambua umuhimu wa siasa katika kukuza maendeleo.

Amesema nchi nyingi Duniani huingia katika migogoro ya kisiasa hali inayopelekea kuleta machafuko ni kwasababu hawana Elimu ya amani na hawajui umuhimu wa uzalendo katika nchi.

Mratibu wa Ofisi ya Mashariki Antony Mkama amesema Tanzania ni nchi ambayo inaelekea Uchumi wa Kati ifikapo 2025 hivyo inahitaji uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali Duniani katika kukua kiuchumi hivyo amani huleta mshikamano ukuaji maendeleo ya kiuchumi.

Charles Mkuvasa ni Afisa mahusiano Africa Mashariki wa Shirika la Elimu ya Amani amesema Africa Kusini walikuwa na migogoro ya kuchomana Moto alienda kama mwakilishi Africa Kusini kutoa Elimu ya amani na walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani watu waliacha kuchomana moto.

Hata hivyo Shirika la Elimu ya amani limejipanga kikamilifu kufikisha elimu ya Elimu nchini na mataifa mbalimbali ikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi, Africa Kusini na Uganda na ulimwenguni kote ili kuwarithisisha mataifa mengine amani iliyopo nchini.

Post a Comment

0 Comments