Na
Amiri kilagalila,Njombe
Mwenyekiti
wa halmashauri ya mji wa Njombe Edwin Mwanzinga ambaye pia ni diwani (CCM) kata ya Matola ameshangazwa na watu
wanaosubiri serikali kutangaza kufunga makanisa wakati tahadhari dhidi ya
maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) zilikwishatolewa.
Mwanzinga
amesema anaamini wananchi wanaelewa taratibu za kujikinga dhidi ya virusi hivyo
ikiwemo kuepuka mikusanyiko lakini anashangazwa kuona watu bado wanakwenda
makanisani wakisubili serikali kufunga makanisa.
Ameyasema
hayo mbele ya waandishi wa habari walipofika ofisini kwake ili kupata maoni
upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujikinga na Corona hususani Barakoa kwa mji wa
Njombe hasa katika kipindi hiki cha mlipuko.
“Mimi
ni imani yangu kubwa kwamba wananchi wanaelewa tahadhari kwamba mikusanyiko
haitakiwi,sasa wewe unaenda kwenye baa ,kwenye mikusanyiko kufanya nini? kama
unaamini kabisa kanisani kuna mkusanyiko kwanini usikae nyumbani kwako ukaomba,sasa
wanataka serikali mpaka itangaze kufunga makanisa,kufunga masoko”alisema
Mwanzinga
Kuhusu
swala la Barakoa Mwanzinga amesema inawezekana ikawa ni changamoto kwa kuwa
awali hazikuwa na matumizi makubwa mitaani.
“Kwanza
mwanzo hatukuwa na hivyo vitu na kama vilikuwepo basi walikuwa wanavaa walioko
kwenye fani ya afya au kilimo ndio walikuwa wanavaa barakoa,lakini sahizi
nimeona nyingi hata za kawaida zinatengenezwa kwasababu swala ni kuzuia mate
yako unapoongea yasiruke kwa mwenzangu,na ninadhani wafanyabiashara kwa sasa
wameanza kuziingiza kwa wingi”alisema Mwanzinga
Winfrida
Mtete Onesmo Mwajombe na Stanley Nyatto ni Baadhi ya wakazi wa Njombe mjini ambao
wengine wamekutwa wakiwa wamevalia
Barakoa na wengine wakisema muda bado kwa Njombe kuanza kuzivaa.
Wauzaji
wa maduka makubwa ya dawa mhimu za binadamu mjini Njombe akiwemo Prisca
Mwanyika wanakiri kuwapo kwa uhaba wa vifaa vya kujikinga na Corona Kama Hand
sanitizer,Barakoa na sabuni na kwamba kutokana na mikoa Jirani ya Ruvuma na
Mbeya kuripotiwa visa vya wagonjwa wa homa ya mapafu uhitaji wa vifaa hivyo umeanza
kuwa mkubwa.
“Sisi
tunaomba tupunguziwe bei hizi barakoa kwasababu upatikanaji wake ni mgumu sisi
tunapata kidogo kidogo kwasababu ukitaka mia mtu anakupa 30 anasema hazitoshi
anauza reja reja yeye mwenyewe,na sasa hivi boksi moja lenye barakoa 50
zinauzwa laki moja laikini uhitaji wa wateja hapa Njombe ni mkubwa tunashindwa
sisi na serikali yetu isiangalie upande mmoja huku kusini tunasahaulika”alisema
Prisca Mwanyika
Ripoti
za wagonjwa wa Corona Nchini kutokana na
taarifa ya wizara ya afya Tanzania hadi sasa wagonjwa wanaotokana na virusi vya
Corona wamefikia 254,vifo 10 na waliopona
ni 11.
0 Comments