TANGAZA NASI

header ads

YANGA KUIFUATA RIVERS UNITED SIKU YA IJUMAA

 



Kikosi cha klabu ya Yanga SC kinataraji kuelekea nchini Nigeria siku Ijumaa kwa ajili ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya barani Africa dhidi ya Rivers United. 

Akizungumza maandalizi ya safari hiyo, Afisa habari wa klabu ya Yamga, Hassani Bumbuli amesema kwamba katika safari hiyo wanataraji kua na msafara wa watu 90 wakiambatana na baadhi ya mashabiki.

Bumbuli amesema kwamba licha ya mechi za awali kutoruhusiwa kuingia mashabiki lakini kwa upande wa klabu wanaruhusiwa kuingia na watu wasiozidi 150 katika mchezo huo utakaopigwa Septemba 19 nchini Nigeria.

Utakumbuka katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Septembe 12, 2021 Yanga ilipokea kichapo cha bao 1-0.

Post a Comment

0 Comments