TANGAZA NASI

header ads

Wanasayansi Kufufua Aina Ya Tembo Waliotoweka Duniani

 



Wakati dunia bado ikiendelea kuuguza kidonda cha COVID-19 huku nchi zingine zikiendelea kupoteza raia wake, wataalamu wa sayansi ya vinasaba kutoka chuo kikuu cha Havard siku ya jumatatu walikubaliana kufanya utafiti uliopewa jina la 'Colossal' ili kurudisha duniani viumbe waliotoweka.

Wanasayansi hao akiwemo mwanabaiolojia Dr George Church wamefanya utafiti na kugundua kuwa wanaweza kuwarudisha duniani aina ya tembo waliokuwa wakubwa zaidi ya tembo wa sasa na manyoya mengi mithili ya sufi na kupewa jina "Woolly Mammoth" walikuwa na uzito wa hadi kufikia tani 10 kwa Mammoth mmoja ambao ni uzito wa kama tembo wawili wakubwa wa sasa.

'Tembo' hao ambao walitoweka duniani miaka 10,000 iliyopita kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kwani walikuwa wanaishi kwenye sehemu zenye baridi kali kama Siberia, Hong Kong ambapo mabaki ya Mammoth mchanga yalipatikana.

Kampuni itakayojishughulisha na utafiti huo tayari imepewa dola milioni 15 za kimarekani kama kianzio na madaktari hao wamesema kuwa, kijusi cha wanyama hao kinatarajiwa kuwa tayari baada ya miaka 6 ambacho kitawekwa kwenye mfuko wa uzazi utakaofanana sana na mfuko wa uzazi wa Mammoth wa enzi hizo.

Dr Church alieleza kuwa, watachukua sampuli za tembo wa sasa na kuzipeleka maabara kisha kuziongezea vina saba vingine kama vya manyoya na uwezo wa kuzalisha mafuta kwa wingi kwani Mammoth walikuwa na mafuta mengi yaliyowasaidia kustahimili baridi kali.

"Hii ni hatua kubwa kwetu, utafiti huu utaleta mabadiliko makubwa" amesema Dr Church.

Kwa upande mwingine, baadhi ya watafiti wameonyesha kutokubaliana na mpango huo na kuhoji maswali kadhaa ikiwemo, ni sahihi kuwarejesha viumbe hao duniani wakati hatuna taarifa za kutosha kuhusu maisha yao?, Je nini kitatokea kama wanyama hao watatishia amani na maisha ya viumbe hai wengine kama binadamu?

Lakini Dr Church amewaondoa hofu na kuwaambia kuwa wanyama wale ni hazina kwa mazingira, kwani wanatunza mazingira na kutoa mbolea na kuongeza kuwa, mpango huo hautakuwa rahisi, lakini mpaka sasa wamepata karibu kila wanalohitaji.

Inakadiriwa kuwa kufikia mwaka 2027 wanyama hawa watakuwa tayari wamerudishwa duniani kupitia utafiti huo na utafiti kuhusu kuongeza wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka kama vifaru weupe na panda bado unaendelea kwa kutumia njia hiyo hiyo ya maabara.

Post a Comment

0 Comments