Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny anayefahamika kama Fahyma amesema kuwa wanaume wengi wa Tanzania wanapenda kuingia kwenye mahusino ya kimapenzi na wanawake pasipo kuwa na malengo ya kufunga pingu za maisha (Ndoa) zaidi ya kuwachezea na kuwacha.
Fahyma amendelea kusema kuwa wanaume ni watu wasio na huruma na kuwashauri wanawake kuacha tabia ya kuwaamini sana wanaume kiasi cha kuwapa thamani ya kupitiliza.
"Wanaume wengi wa Tanzania wanapenda sana kuwachezea wanawake na kuwaacha pasipo na kuwa na malengo kabisa"
"Wanawake wenzangu tuache kuwaamini sana kiasi cha kuwapa moyo wa thaman na kupitiliza ni watu wasio na huruma kabisa na sisi bora kuwa single na kutengeneza maisha na thamani yako katika jamii" amesema Fahyma.
Watu wengi katika mitandao ya kijamii wamepokea kauli hiyo ya Fahyma kama dongo kwa Paula Paul ambaye kwa sasa yupo kwenye mahusino ya kimapenzi na Rayvan ambaye ni mzazi mwenza.
Fayhma na Rayvanny walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume anayejulikana kwa jina la Jayden.
0 Comments