TANGAZA NASI

header ads

Mwanza:Waandishi wa habari wahimizwa kutoa maoni yatakayowapa uhuru wa kufanya kazi



Na Maridhia Ngemela

Waandishi wa habari Mkoani Mwanza leo hii wamefanya mkutano wa  mchakato wa kutoa  maoni juu ya kutengeneza kanuni za madili ya uwandishi wa habari.

 Mkutano huo umeandaliwa na chama cha waandishi wa habari  Mkoani Mwanza (mpc) chini ya ufadhili wa mradi wa ushirikiano Kati ya  Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania ( Utpc) na international Media support ( Ims) ikiwa na lengo la kuwapa waandishi nafasi ya kutoa maoni juu ya kanuni za madili ya uwandishi wa habari.

Meneja mradi wa mafunzo,utafiti na machapisho Victor Maleko kutoka Utpc amesema kuwa,kulikuwa na wimbi kubwa la waandishi wa habari kukamatwa hovyo , tunatengeneza mazingira mazuri ili kujikinga zaidi kuliko Serikali kuja kuweka mkono ni vema itukute tushajiwekea ulinzi na tufuate kanuni ambazo leo hii tunazitolea maoni kwa lengo la kutulinda katika taalum yetu.

Mwenyekiti  mstaafu wa Chama cha waandishi wa habari Mkoani Mwanza (mpc) Osoro Nyawangah amesema chimbo cha habari au mwandishi wa habari ni mtu wa kipekee ambae anapata fursa ya kuzungumza na viongozi mbalimbali amewataka waandishi kusimamia  sheria,kanuni na taratibu ambazo wamezitolea maoni wenyewe ili iwe ni taalum yenye tija.

"Nyawangah amesema tunayotaaluma ambayo tukiifanyia kazi vizuri inaweza kubadirisha Nchi yetu bila kumsukuma mtu yeyote ,tunaowajibu mkubwa Sana kuibadirisha na kuisukuma jamii  kuwa masikini au tajili "amesema Nyawangah

Pili mtambaliki aliyekuwa muwezeshaji katika mkutano huo amesema ni vema kuendelea nikumbusha kanuni na sheria katika taalum ya uwandishi wa habari ili kuepukana na msuguano ikiwemo usumbufu unaojitokeza mara kwa mara katika vyombo vya habari.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpc Edwin soko amewataka waandishi kuwa makini katika mafunzo watakayoyapata na kutoa mapendekezo mazuri ili kuondoka shida zinazoweza kujitokeza hapo mbeleni za kuvutana na dola.

Soko ameishukru Utpc kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ambayo yanaandaliwa kwa lengo la kuendelea kuwakumbusha wanataaluma juu ya sheria ambazo zinatakiwa kuzingatiwa katika ufanyaji kazi wa mila siku ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments