TANGAZA NASI

header ads

CDF Mabeyo azindua eneo la Burudani la JKT Jijini Dodoma na ukumbi Mkubwa eneo litakalo kuwa na burudani mbalimbali

 


Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amezindua eneo la burudani na ukumbi wa kisasa wa burudani wa Jeshi la kujenga Taifa JKT  lililopo eneo la Medeli East Jijini Dodoma ikiwa ni kitega uchumi kwa JKT huku akiwataka JKT kuzingatia huduma bora na ubunifu kwa wateja kuvutia watu zaidi.

Akizungumza mara baada ya kuzindua ukumbi huo wa burudani wenye uwezo wa kubeba watu 1000 hadi 1200 kwa pamoja na kuwa na burudani mbalimbali amesema jengo hilo ni ubunifu mkubwa hivyo inatakiwa litunzwe ili liwe endelevu sambamba na kutoa huduma bora.

“Niwapongeze JKT kwa ubunifu huu kwanza wametimiza agizo la Serikali na mimi binafsi niliagiza majeshi yaanze kujitegemea bila kutegemea bajeti ya serikali na hapa naona huu ni ubunifu mkubwa naamini mtafikia lengo hilo” amesema.

Amesema alitoa agizo la kubuni miradi na wengi naona wanabuni vizuri hasa katika kilimo na ufugaji jambo ambalo litasaidia kwa majeshi kujitegemea na ninaomba miradi hiyo iwe endelevu na ili kufikia pia lengo la kuhakikisha kuna kuwa na usalama na uhakika wa chakula.

Amewataka kuwa wabunifu zaidi kwani fulsa zipo nyingi ambazo zinaweza kuwanufaisha katika kilimo na ufugaji kwani bado kuna ardhi ya kutosha ambayo itawezesha kupatikana kwa mapato ya wao kujitegemea na kuhakikisha wanakuwa na miradi mingi inayozalisha.

Pia amewataka kukamilisha kwa wakati baadhi ya majengo ambayo bado ambayo yatafanya kukamilika kwa mradi huo ikiwamo kumbi ndogo na maeneo mengine yanayokamilisha mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema mradi wa eneo hilo ya Burudani ni katika kutekeleza maagizo ya kuhakikisha jeshi hilo linajitegemea na mradi huo ni sehemu ya miradi mingi waliyoibuni ikiwamo ya kilimo, Ufugaji na Uvuvi na watahakikisha wanaisimiamia miradi hiyo kikamilifu ili iwe endelevu.

Amesema mpaka sasa wana mashamba na skimu za umwagiliaji Chita Morogoro na mashamba ya mazao Mahindi na Maharage mikoa ya nyanda za juu kusini na mkoa wa Katavi na wameanza kujihusisha na kilimo cha mda mrefu na mfupi.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mkuu wa tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa JKT. Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema mradi huo ulianza mwaka 2018 katika ujenzi wake na eneo hilo lina ukubwa wazaidi ya  ekari 2 na kutakuwa na burudani za aina nyingi ikiwamo huduma za ukumbi.

Amesema eneo hilo la burudani litatumiwa na maafisa, askari , watumishi wa umma na wananchi kama sehemu ya burudani ambapo kutakuwa na burudani nyingi ikiwamo live bendi na michezo ya watoto na huduma mbalimbali zitapatikana.

Aidha amebainisha kuwa mpaka sasa miondombinu ya eneo hilo imetumia bilioni 1.9 ikiwa ni ujenzi wa jingo la utawala, ukumbi, uzio na taratibu za ujenzi pia kwa majengo ambayo hayajajengwa yatagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.2 na kwa ujumla miondombinu hiyo itagharimu zaidi ya bilioni 3.1.

Amebainisha kuwa JKT wapo tayari kupokea mapendekezo mbalimbali yatakayotolewa na wadau ili kuboresha zaidi huduma katika eneo hilo ili liweze kuvutia zaidi na mara baada ya kuzinduliwa na Mkuu wa majeshi ukumbi utakuwa tayari kwa kupokea ada ya matumizi ya ukumbi hupo kwa shughuli mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments