Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameongoza shughuli ya kuaga mwili wa Mbunge wa Ushetu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandikwa, aliyefariki dunia Agosti 2 wakati akiendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili
Amesema, "Nilifanya ziara nikifahamu namuacha Kwandikwa akiwa anaugua Natoa pole kwa familia, Chama cha Mapinduzi, Bunge, wananchi wa Ushetu, watumishi wa Wizara ya Ulinzi pamoja na wananchi wote. Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu,
Kifo cha Waziri Elias Kwandikwa ni pigo kwa familia na Serikali, nilipata taarifa nikiwa ziarani nchini Rwanda nikiwa na Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Paul Kagame hivyo nae amenituma niwape pole Watanzania wote" - Rais Samia Suluhu Hassan
0 Comments