Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baraza la madiwani halmashauri ya
wilaya ya Njombe limeagiza ofisi ya mkurugunzi kufanyia marekebisho ya sheria ya tozo ya ushuru wa mbao na mkaa ili
kuvutia wafanyabiashara wengi pamoja na
wale ambao wamefika hatua ya kuhama kufanyabiashara katika halmashauri hiyo.
Katika mkutano wa baraza la madiwani
halmashauri ya wilaya ya Njombe baadhi ya madiwani akiwemo Javan Ngumbuke na Roida
Wandelage wamesema kumekuwapo kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaotoroka kununua
mbao na mikaa katika maeneo yao kutokana na tozo kubwa jambo linalokwamisha
jitihada za ukusanyaji mapato.
“Watu wengi wanalalamika kwamba ushuru
ni mkubwa na hata hapa Mtwango tulikuwa na wafanyabiashara wengi wa mbao sasa
kwasababu ya ushuru mkubwa wamehama wanaenda knunua mbao halmashauri ya mji na
wengine wameacha kabisa biashara hiyo na kuingia kulima mahindi wanadai ni bora
kulima mahindi kwasababu ushuru ni naafuu kuliko ushuru wa mbao”alisema Roida
Wandelage
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Valentino
Hongoli amesema licha ya kufanikiwa kuvuka lengo katika makusanyo ya ndani
lakini tozo kubwa zilizowekwa kupitia sheria ndogondogo zimesababisha baadhi ya
wafanyabiashara wa mbao na mkaa kukimbilia katika halmashauri nyingine jambo
ambalo ni lazima kubadilishwa kwa kanuni za tozo hizo.
“Kwa kuwa kilimo cha wafanyabiashara
wetu wa mbao na mkaa ni kuwa halmashauri yetu tunachaji ushuru mkubwa mno
tofauti na halmashauri nyingine,Niagize kupitia baraza hili kwako wewe na CMT
yako mfanye mchakato wa haraka ili tuweze kufanya marekebisha ya hiyo sheria
kwasababu ikifanyiwa marekebisho itawavutia wafanyabiashara wengi kuingia
kununua mbao na mkaa katika halmashauri yetu hali ambayo itapandisha sana
kupunguza na watu kukwepa mapato”alisema Valentino Hongoli
Kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Njombe,katibu
tawala wa wilaya hiyo Emmanuel George amesema pamoja na jitihada
kubwa zinazofanywa katika ukusanyaji mapato ya ndani lakini fedha hizo zisaidie
katika kukamilisha maboma yaliyojengwa kwa kushirikiana na wananchi.
“Tuhakikishe tunakusanya mapato ya
kutosha ili yaweze kufanikisha shughuli zingine za serikali lakini pia
tunapokusanya vizuri tuhakikishe tunapeleka fedha kwenye miradi hususani
umaliziaji wa maboma maana yake tuanokusanya vizuri pia tunapeleka fedha kwenye
miradi vizuru”alisema Emmanuel George
Baadhi ya wafanyabiashara wa mkaa na
mbao akiwemo Juma Augustino na Isaya Kaduma wamesema tozo hizo zimewafanya
kuporomoka kiuchumi kutokana na tozo hizo kutoendana na soko la bidhaa za
misitu ya mbao kitaifa na kimataifa.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Njombe bwana Lukelo Mshaura amekiri kupokea maagizo hayo na kwamba atakwenda
kuyafanyia kazi.
“Tuhakiksha mchakato unapita katika
maeneo yote yanayotakiwa kupita ili tuhakikishe tunakuja na kitu ambacho ni
msaada kwa wananchi lakini pia tumeshaiona changamoto hiyo na kujikita pia
kutafuta vyanzo vingine endelevu,sisi tumeupokea huo ushauri na kuufanyia
kazi”alisema Lukelo Msahura
Halmashauri hiyo inatajwa kutoza ushuru
wa shilingi 200 kwa kila ubao huku halmashauri zingine zikitoza shilingi
100.Hata hivyo licha ya changamoto hizo lakini katika makusanyo ya ndani
halmashauri ya wilaya ya njombe imefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo kwa kukusanya zaidi ya asilimia 111.
0 Comments