Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewauwa wapiganaji wasiopungua 78 ambao imewaita kama wanachama wa makundi ya uhalifu wakati wa shambulio la angani kwenye maficho yao kaskazini magharibi mwa nchi.
Wapiganaji wengi waliuawa wakati wakijaribu kutoroka mashambulio ya angani kutumia pikipiki, afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la angani Edward Gabkwet alisema Katika wiki za hivi karibuni vikosi vya usalama vya Nigeria vimeimarisha operesheni dhidi ya wanamgambo wenye silaha.
Wanamgambo hao wamewateka nyara zaidi ya wanafunzi 1,000 kutoka shule na vyuo tangu Desemba iliyopita. Karibu watoto 300 wa shule bado wameshikiliwa mateka .
Mamlaka za Nigeria zimekosolewa kwa kushindwa kumaliza ghasia ambazo pia zimesababisha maelfu ya watu kuuawa .
Siku ya Alhamisi, Amnesty International ilitaka haki iwepo katika kesi dhidi ya mtu yeyote anayetuhumiwa kwa vurugu.
0 Comments