TANGAZA NASI

header ads

Njombe:Wadau wa chai wazidi kupata elimu kufikia kilimo endelevu

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Pamoja na jitihada zinazochukuliwa na wadau pamoja na serikali katika kuinua sekta ya chai nchini lakini bado tasnia hiyo inakwamishwa na miundombi up duni ya barabara zinazoelekea maeneo ya uzalishaji pamoja na bei ndogo ya majani ya chai kutoka kwa wakulima.


Ripoti za serikali zinasema mwaka 2018 na 2019 uzalishaji wa malighafi hiyo ulipanda lakini ukashuka tena 2020 huku sababu nyingine zikiorodheshwa ikiwemo ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona Uliyosababisha kuyumba kwa soko la kidunia.


Wakizungumza mara baada ya mafunzo ya IMS yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uendeshaji wa mifumo ya kisasa katika viwanda na makampuni ya chai kwenye semina ya siku tatu chini ya mradi wa Mark Up kwa ufadhiri wa umoja wa ulaya akiwemo Boaz Malekela na Michael Briton wanasema mafunzo hayo yatasaidia kukuza sekta ya chai huku wakiomba mradi huo kuona namna ya kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya barabara siku za mbeleni.



“Mafunzo haya ya kilimo endelevu yanatusaidia sana sisi kutuelekeza nini cha kufanya kwasababu kwenye makampuni tunapata tabu ya kumiaraisha mfumo,kwa hiyo tunaamini yanatusaidia zaidi kuandaa mfumo wa kilimo endelevu kwa wakulima kwa hiyo kwasababu sisi tunawasimamia wa kulima hivyo ni lazima tuwaongoze “Alisema Boaz Malekela  Msimamizi wa mfumo endelevu kutoka kampuni ya Nosc


Aidha amesema Sekta ya Chai kwa mkoa wa Njombe inaendelea kukua kwa kasi kutokana na juhudi za wadau na serikali hivyo ametoa rai kwa serikali kuboresha zaidi katika changamoto za miundombinu ya barabara kutoka mashambani kuelekea viwandani ili kuokoa uharibifu wa zao hilo.


Naye Michael Briton kutoka umoja wa wasimamizi wa mfumo endelevu kwa wakulima wadogo wa Chai Rungwe waanamini katika semina hiyo wanakwenda kuongezewa uwezo katika utekelezaji wa kanuni na standard za kilimo endelevu.


“Katika maeneo yetu wakulima wengi bado wanalalamikia bei ya chai kwamba imekuwa ikipanda taratibu sana kwa hiyo inachangia vijana wengi kuto hamasika kwenye kilimo cha chai na kurudisha nyuma dhana ya kilimo endelevu,tunaamini malengo haya yatafikiwa kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na wadau wa chai kwa kushirikiana na serikali”alisema Michael



Akiezeleza sababu ya kutoa mafunzo ya IMS kwa wamiliki wa viwanda na makampuni yanayojihusisha na sekta ya chai nchini Christian Sakarani ambaye ni mshauri wa mradi anasema ni kuboresha uendeshaji wa makampuni hatua ambayo itasaidia sekta ya kuzidi kuimarika kila siku  sambamba na kukidhi mahitaji ya maendeleo ya teknolojia ya sasa.


“Lengo la kufanyika kwa haya mafunzo ni kuweza kusaidia ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa na kumekuwa na mahitaji makubwa sana kutoka kwa watumiaji wa mazao kwa hiyo tunataka kuhakikisha toka kuanzishwa kwa hili zao  mpaka linamfikia mtumiaji basi hapa kati kati pasiwe nachangamoto kabisa”alisema Christian Sakarani


Awali akifafanua faida ya kuwa na mfumo mmoja utakaokusanya mifumo yote ya uendeshaji na namna utakavyopelekea sekta hiyo kupiga hatua mkufunzi wa mafunzo hayo Gitau Wamukui anasema itapunguza usumbufu na gharama zisizo za lazima huku Robert Charles ambaye ni mkaguzi wa bodi ya chai Mufindi anasema suala la mbolea na masoko vihimarishwe zaidi ili mkulima apate tija.


Zaidi ya wajasiliamali wakati na wadogo 20 kutoka maeneo ya wazalishaji wa Chai Tanzania,wameweza kuhudhuria hatua ya kwanza ya mafunzo ya uzalishaji wa zao la chai yanayotolewa mkoani Njombe kupitia kituo cha uwekezaji ITC.

Post a Comment

0 Comments