TANGAZA NASI

header ads

Bodi ya korosho yawaonya waendesha maghala



Na Ahmad Mmow, Lindi. 

 Waendesha maghala waliopewa dhamana ya kuhifadhi korosho wametakiwa kuwa waaminifu ili kulinda ubora wa korosho na kuepuka kusababisha migogoro. 

 Agizo hilo lilitolewa jana na mkurugenzi wa bodi ya korosho, Fransis Alfred  kijijini  Lihimalyao, tarafa ya Pande, wilaya ya Kilwa wakati wa uzinduzi wa mpango wa ugawaji  pembejeo kwa wakulima wa korosho. 

 Mkurugenzi huyo wa bodi alisema changamoto iliyopo maghalani haisababishwi na majengo ya maghala bali usimamizi wa waliopewa dhamana ya kuendesha na kusimamia. ¥ Alisema baadhi ya waendesha maghala sio waaminifu.

 Kwani wanabadilisha na kuharibu ubora wa korosho za wakulima zinazopelekwa na vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kwenye maghala wanayoendesha. 

Alfred ambaye bodi anayoongoza inaratibu na kusimamia mpango huo alisema baadhi ya waendesha maghala wanabadilisha ubora wa korosho za wakulima kutokanana tamaa. 

Huku wakijua kwamba kitendo hicho nikosa na kinasababisha migogoro baina ya wakulima na serikali, wakulima na vyama vikuu na hata AMCOS na wakulima. ¥ Kutokana na ukweli huo, alisema bodi haitawavumilia waendesha maghala wa aina hiyo. 

Huku akiweka wazi kwamba katika msimu wa 2021/2022 bodi hiyo itafanya mabadiliko ya waendeshaji maghala. Ikiwemo ghala la Nangurukuru lililopo wilayani Kilwa. 

 Aidha mkurugenzi huyo aliwataka viongozi wa vyama vya ushirika  kusimamia  kikamilifu maghala ambayo yanahifadhi korosho zawakulima. 

 '' Viongozi wa vyama vikuu timizeni wajibu wenu kikamilifu. Mnatugombanisha nawakulima,'' alisema Alfred.  

 Awali baadhi ya wakulima wakiwamo Seleman Chande, Hadija Hassan na Said Omari waliiomba serikali iwaruhusu wajenge ghala la kuhifadhia mazao katika tarafa ya Pande  ili ununuzi ufanyike kwenye ghala hilo badala ya Nangurukuru. 

Wakulima hao walisema hawaridhishwi na ghala la Nangurukuru. Kwamadai kwamba linawasababishia hasara kutokanana kuingizwa korosho chafu zinazoharibu ubora wa korosho zao. ¥ Uzinduzi huo ulikuwa wakitaifa. 

Ambapo zoezi la ugawaji wa pembejeo kwawakulima wakorosho litaendelea nchi nzima. Huku ikielezwa kwamba zoezi hilo litakwenda sambamba na utoaji mafunzo kwa wakulima ya jinsi ya kutumia viwatilifu. Mafunzo ambayo yatatolewa na taasisi ya utafiti wa mazao ya kilimo kituo cha Naliendele( TARI-Naliendele).

Post a Comment

0 Comments