TANGAZA NASI

header ads

WANGING'OMBE:Wanawake na watoto wawekwa kizuizini zaidi ya masaa 9 kwa kukosa mchango wa shule



Na Clief Mlelwa,Wanging'ombe

Wananchi wa kijiji cha luduga kilichopo wilaya ya wanging'ombe mkoani Njombe wamelalamikia kitendo cha viongozi wa kijiji hicho kuwakamata na kuwaweka ndani ya ofisi kina mama wakiwa na watoto wadogo kwa tuhuma za kutolipa mchango wa ujenzi wa shule ya sekondari. 

Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa licha ya kuwa na matatizo ya kiafya na kuwa na watoto wadogo bado viongozi hao wamewakamata na kuwafunga kwa zaidi ya saa 9.

Akizungumzia kuhusiana na malalamiko hayo mwenyekiti wa kijiji hicho  AMADY OMARY MPANYE  amekiri kuwepo kwa zoezi hilo la kuwakamata wale wote ambao hawajalipa mchango na kueleza kuwa hajapokea changamoto ya wananchi hao wanaodai wamefungwa wakiwa na watoto wadogo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Luduga Hassan Ngella amesema kuwa hana taarifa ya wananchi hao kufungwa wakiwa na watoto wadogo na wenye matatizo ya kiafya na kuwataka kuendelea kutoa mchango wa ujenzi wa shule ya sekondari ya luduga.

Post a Comment

0 Comments