TANGAZA NASI

header ads

Rais Samia :Hayati Magufuli aliniamini na kumeniwezesha kuwa Mwanamke wa Kwanza Tanzania kushika nafasi ya Umakamu wa Rais na hatimaye sasa Rais

  


“Niseme wazi kuwa uwezo wangu uliibuliwa na Mh Amani Abeid Karume aliyenipa nafasi ya uwaziri katika kipindi changu cha awali na cha pili nikiwa mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar.


"Maelezi haya yaliendelezwa na Mh Jakaya Kikwete aliyenipa uwaziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baadaye kuniamini kwenye nafasi ya kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la katiba, fursa hii ilinipa nafasi ya kuwajua na kufanyakazi na baadhi yenu humu ndani na ndiyo fursa iliyonitambulisha kwa watanzania.

"Nimshukuru sana ingwa hatuko naye duniani, Hayati Dk. John Magufuli kwa kuniamini kuwa mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 na 2020, kuniamini kwake kumeweza kunifanya kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika wadhfa wa Makamu wa Rais na hatimaye sasa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,” Rais Samia Suluhu.

Post a Comment

0 Comments