“Ndani ya nchi yetu kumekuwa na mzunguko mkubwa watu wanapokuja kutaka kuwekeza, serikali ya wamu ya sita tunakwenda kukosesha hilo na uwekezaji sasa utakwenda kufanyika kwa haraka, kutakuwa na sifa na matakwa maalumu yatakayowekwa kwa uwazi katika kutambua miradi ya kimkakati itakayostahiki vivutio vya kikodi au vivutio vinginevyo.
“Suala la upatikanaji wa mitaji nalo halinabudi kuangaliwa kwa umakini mkubwa, kama mnavyofahamu ili sekta binafasi iweze kustawi vizuri hatuna budi kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara.
“Nchi yetu imekuwa ikilalamikiwa kwa kutokuwa na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ikiwamo kutokuwa na na sera zinazotabirika, utaratibu wa kodi usio na utulivu, urasimu mwingi katika kutoa huduma kwa wawekezaji na matatizo mengine nayaikwamisha ustawi wa biashara na uwekezaji, hivyo serikali ya awamu ya sita inakusudia kufaya maboresho makubwa," Rais Samia Suluhu.
0 Comments