TANGAZA NASI

header ads

Ndugai atoa ushauri kukosekana kwa dawa



 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema suala la kukosekana kwa dawa mahospitalini ni la muda mrefu hivyo ameiomba Wizara ya Fedha na Mipango kuchukua deni la Bohari ya Dawa nchini (MSD) ilikusaidia upatikanaji wada.


Mhe. Ndugai amesema hayo leo Bungeni Dodoma kabala ya kuhairisha mkutano wa bunge ili kutoa fura kwa shughuli ya viapo kwa mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hapo jana.


"Suala la kukosekana kwa dawa sio la jana au juzi, ni la siku nyingi kila tukikaa MSD hivi kwanini wizara ya fedha msichukue hilo deni la MSD ili fedha zinazopelekwa MSD zitoe dawa, na nyinyi mtajuana na MSD kwa aina yenu," alisema Mhe. Ndugai.


Pia Spika Ndugai amewapongeza viongozi walioteuliwa hususani mawaziri na wale walioendelea kubakia kwenye nyadhifa za uwaziri huku akiwasisitiza wasikilize ushauri wa wabunge kwani wanaongea kwa niaba ya Wannachi.


"Yapo mambo mengi yakufanya kila mmoja kwenye wizara yake na mengi sana mtayapata kama ushauri kutoka kwa wabunge cha msingi nyinyi ni wabunge kama sisi, hapa bungeni ndio nyumbani huko mmeenda kama matembezi," alisema Mhe. Ndugai.


Mikutano ya bunge, kipindi cha maswali na majibu umesitishwa kutokana na shughuli za kuapishwa kwa mawaziri baadae hii leo pamoja na Sikukuu za Pasaka hivyo bunge litaendelea tena na vikao vyake siku ya Jumanne tarehe 6/04/2021.

Post a Comment

0 Comments