TANGAZA NASI

header ads

Wandamanji wakabiliana na polisi Uingereza

 


Polisi mjini Bristol nchini Uingereza wamewakamata watu 10 wakati wa maandamano ya usiku yaliyodumu kwa siku tatu kupinga sheria mpya ya polisi. 


Mamia ya waandamanaji wanapinga mswada juu ya mahakama unaohusu polisi, uhalifu, na hukumu. Mswaada huo uliowasilishwa bungeni unalenga kuwapa polisi mamlaka na nguvu zaidi katika kuzuia maandamano. 


Jeshi la Polisi la Avon na Somerset limesema waandamanaji waliwarushia polisi mayai, chupa, mawe pamoja na kumpaka rangi farasi wa polisi. 


Mkuu wa Polisi, Mark Runacres amesema maafisa walionyesha uvumilivu kwa kiwango cha juu na walitumia nguvu kwa kiasi kinachofaa. Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amekosoa vikali mashambulio hayo aliyoyataja kuwa ya aibu dhidi ya polisi. 


Maadili ya polisi na vipaumbele vyake nchini Uingereza yamekuwa katika uchunguzi mkali kufuatia kifo cha Sarah Everard, mwanamke mwenye umri wa miaka 33 ambaye alitoweka Machi 3. Afisa wa polisi anayehudumu alishtakiwa kwa mauaji ya mwanamke huyo.

Post a Comment

0 Comments