Na Amiri Kilagalila,Njombe
Madereva wa jinsia ya kike wanatajwa kuwa na uwezo
mkubwa wa kuchukua tahadhari na kuepuka ajali za barabarani ukilinganisha na
wanaume kutona na ajali ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara huku sababu
mbali mbali ikiwemo kujiamini kupita kiasi,ulevi na uzembe vikitajwa chanzo cha
ajali za barabarani zinazosababishwa na wanaume.
Mkufunzi kutoka chuo cha Taifa cha usafirishaji
mwalimu Frolian Alexanda Sonya amebainisha hayo mara baada ya kukamilisha usimamizi
wa mitihani kwa madereva zaidi ya 20 wa magari waliokuwa wakipata mafunzo katika
chuo cha udereva mpechi kilichopo Uwanja wa sabasaba mjini Njombe ambacho
kinatoa elimu kwa wamiliki na wasafirishaji wa vyombo vya moto.
“Dereva wa kike umakini wao barabarani upo juu sana
lakini walio wengi hawajiamini na laiti tungeweza kutoa mafunzo kwa jinsia hii
kwa kiasi kikubwa pengine hizi ajali barabarani ingekuwa ni za kuskia tu,na
mpaka sasa si chini ya wanawake 400 tumeshaweza kuwajengea uwezo kwasababu
umakini wao ni wajuu sana ukilinganisha na wanaume”alisema Frolian Alexanda
Sonya
Aidha amewataka madereva wakiwemo wa abiria
kuendelea kupata elimu ya kujitambua na kujiheshimu pamoja na kubadilika kitabia
ili kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na wakati mwingine kuepuka kusababisha
ajali zinazoweza kuepukika
Mkurugenzi wa chuo cha udereva Mpechi mjini Njombe
Bi. Abiya Mpangile amesema chuo hicho kinaendelea kutoa fursa kwa kila dereva
kupatiwa elimu kabla ya kuendesha vyombo vya moto pamoja na kutoa mchango
katika kutokomeza matukio ya ajali za
barabarani na kutoa wito kwa wamiliki wa magari kuajili madereva waliokwisha
kusoma.
Aidha kuhusu wanafunzi wa jinsia ya kike amesema
chuo hicho kimekuwa kikipokea wanafunzi wa jinsia mbali mbali wakiwemo wa jinsia hiyo huku akipongeza umakini wao
wanapokuwa bara barani.
“Wakina barabarani huwa tunakuwa makini sana tofauti
na hawa wenzetu kwa kuwa kujiamini kwao kunakuwa ni kupita kiasi na mimi
napenda sana wakina mama wangekuwa wamejiunga kwenye hizi kozi tungekuwa tumepunguza
sana ajalia”alisema Abiya Mpangile
Mkuu wa
usalama barabarani Mkoa wa
Njombe Jane Walioba amesisitiza
madereva na wamiliki wa vyombo vya moto ikiwemo wa magari na pikipiki zote
kujiunga na vyuo vya udereva kuepukana na changamoto za barabarani.
Kwa upande wao wahitimu wa udereva magari ya abiria waliofanya
mtihani wao akiwemo Visent Stiven na Noa Kisaika wameahidi kuendesha magari yao
kwa kuzingatia kanuni na sheria za barabarani na kushawishi wengine kujiunga na
vyuo vya udereva ili kutokomeza matukio ya ajali.
“Kwanza ninashukuru kwa hii fursa hapa Njombe
kwasababu miaka ya nyuma haikuwepo,nilivyoona hii fursa nimeona ni chachu ili
kujua sheria kwa upana zaidi.Wito wangu kwa madereva ni kwamba tumemaliza
mafunzo na tunanda kufanya kazi kwa vitendo kwa hiyo ni lazima tukawe watulivu
kwasababu kila gari ina tabia zake”alisema Noa Kisaika






0 Comments