TANGAZA NASI

header ads

Mvua kubwa zasababbisha mafuriko katika Pwani ya Australia



 Mvua kubwa zilizonyesha mashariki mwa Pwani ya Australia mwishoni mwa wiki, zimesababisha mafuriko mabaya katika nusu karne kwenye baadhi ya maeneo na kulazimisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao huku nyumba nyingi zikiharibiwa.

 Waziri mkuu wa New South Wales, jimbo lenye idadi kubwa ya watu nchini Australia, amesema mvua hizo kubwa zilikuwa kubwa kuliko ilivyotarajiwa awali haswa katika maeneo ya chini ya kaskazini magharibi mwa Sydney. 

Watu kadhaa katika sehemu za mji wa Sydney waliamriwa kukimbia nyumba zao katikati ya usiku wakati maji yaliyokuwa na kasi yakisababisha uharibifu mkubwa. 

Picha za kwenye runinga na mitandao ya kijamii zimeonyesha nyumba zikisombwa, miti ikivunjwa na uharibifu wa miundombinu ya barabara. Mamlaka ya hali ya hewa imesema mvua hizo zitaendelea kunyesha kwa siku kadhaa.

Post a Comment

0 Comments