Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo leo Machi 30, 2021 amethibitisha kuwa wanamshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko aliyesimamishwa kazi na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu yanaoendelea kusemwa kuwa walimkamata akiwa anatoroka huku akisisitiza kuwa hatua hiyo ya kushikiliwa ni utaratibu tu wa uchunguzi.
"Hapana sisi hatuna huo ukweli wa kutoroka lakini tumemshikilia kwa sababu ambazo isingekuwa vyema mimi niziongee hapa sasa hivi, lakini ni utaratibu tu wa uchunguzi,'' - Brigedia Jenerali John Mbungo.
Eng. Deusdedit Kakoko alisimamishwa kazi Machi 28, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere na kubaini uwepo wa ubadhirifu Bandarini.
0 Comments