TANGAZA NASI

header ads

Hii hapa ratiba ya Simba kwa mwezi April

 


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba ana kazi ya kufanya ndani ya Aprili kukiongoza kikosi chake kusaka pointi tatu kwenye mechi zake 6 ambazo ni dakika 540 za moto.

Mechi hizo ni dhidi ya AS Vita Club Aprili 3, mchezo wa kwanza walipokutana nchini DR Congo, ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba, Al Ahly ya Misri Aprili 9, mchezo wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly, hizi mbili ni dakika 180 za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa upande wa Ligi Kuu Bara atakuwa na kazi mbele ya Kagera Sugar, Aprili 14, Uwanja wa Kaitaba na mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja Wa Uhuru ubao ulisoma Simba 2-0 Kagera Sugar.

Pia ana kazi mbele ya Dodoma Jiji ni Aprili 18, mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Simba ilishinda mabao 2-1, Coastal Union ni Aprili 25 mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilishinda kwa mabao 7-0.

 Funga kazi kwa Gomes itakuwa ni Aprili 28 dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Simba ilipokutana kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ubao ulisoma Mtibwa Sugar 1-1 Simba.

Gomes amesema kuwa katika mechi zake zote wanahitaji pointi tatu muhimu.

Tayari kikos cha Simba kimeanza mazoezi jana, Uwanja wa Simba Mo Arena kwa ajili ya maandalizi ya mechi hizo ambapo miongoni mwa wachezaji walioanza ni pamoja na Miraj Athuman, Ibrahim Ajibu.

Post a Comment

0 Comments