Rais mstaafu Jakaya Kikwete anasema hayati Magufuli alikuwa rafiki waliyeshibana. "...alipokuwa Waziri wangu, yeye pekee alikuwa anaweza kunitania....Mawaziri wengine walikuwa hawawezi .."
Mstaafu Kikwete anasema urafiki wake na Magufuli ulichagizwa sana na urafiki wa wake wake zao. Mama Salma Kikwete na Mama Janeth Magufuli ni marafiki walioshibana tangu wakati wakiwa wanafundisha kwenye shule moja.


0 Comments