Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameeleza kwa upana jinsi alivyofanya kazi kwa pamoja na hayati Magufuli. Amesema Magufuli alikuwa 'jembe' lake , hivyo alimuweka kwenye Wizara alizohitaji mabadiliko. Alitoa mfano wa Wizara ya Miundombinu, ambapo alimpa jukumu la kuunganisha mikoa ya Tanzania kwa njia ya barabara, kazi ambayo waliikamilisha.
Jakaya anasema, uwezo wa Magufuli katika Uwaziri ulimshawishi kwamba anaweza kuwa Rais na kusema kwamba yeye (Kikwete akiwa Mwenyekiti wa CCM) alipeleka majina matano kwenye chama chake akisema hao wanaweza kuwa Marais. Anasema jina la Magufuli lilikuwa na kwanza.
Kwa namna hiyo, Kikwete amewashangaa watu waliokuwa wanazusha kwamba yeye hampendi Magufuli. "...miiiimiiii?.....Labda JK mwingine.." alisema Kikwete.


0 Comments