Na Amiri Kilagalila
Wakati serikali
ikielekeza nguvu kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na nishati ya umeme,mkoani
Njombe watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika wilaya ya kipolisi
mjini Makambako kwa tuhuma za kukutwa na
nyaya za umeme zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 43 zinazotumika
kusambazia umeme wa mradi wa REA.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema hatua hiyo imekuja baada ya jeshi la polisi
kufanya upelelezi wa kuwanasa watuhumiwa hao, kufuatia aliyekuwa msimamizi wa
mradi wa Rea katika kata ya Kichiwa Tarafa ya Makambako kutoa taarifa kwenye
jeshi hilo alipogundua dram sita za nyaya za umeme zenye thamani ya shilingi
zaidi ya milioni 43 kuibwa .
“Tumekamata gari aina ya fuso na
imebeba waya Rol zipatazo sita na hizi rol zipo nyaya za aina mbili tofauti
zinazotumika kwenye umeme wa rea hapa mkoani Njombe”alisema Hamis Issa
Kamanda Issa amesema
wamefanikiwa kukamata gari hilo kutokana na ufuatiliaji uliofanywa na vikosi
vya polisi.
“Tuliweza kubaini
kutokana na nyaraka iliyodondoka ya faini iliyotozwa hii gari,ikajulikana iko
Dar Es Salaam,amefuatwa tajiri akasema gari iko Katavi na tulipofuatilia
tuliikuta Mlele sehemu moja inatwa maji moto”alisema Kamanda Issa
Vile vile ametoa rai kwa wananchi
kuendelea kuliamini jeshi hilo kwa kuwa lipo imara na watahakikisha jeshi
linalinda miradi yote ya serikali hivyo wananchi wawe tayari kutoa taarifa
miradi inapohujumiwa.
0 Comments