Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameonya na kuwatahadharisha wasimamizi wa wanafunzi watakaothubutu kuchepusha na kuingiza sokoni taulo za kike zilizokabidhiwa kwa shule 24 za sekondari mjini Njombe kwa ajili ya matumizi ya wasichana waliopevuka wanapokuwa hedhi.
Ruth Msafiri ametoa onyo wakati akikabidhi vifaa hivyo vlivyonunuliwa na halmashauri ya mji wa Njombe kwa ajili ya wanafunzi ili kuwasaidia kuongeza muda wa kuhudhuria vipindi darasani pamoja na kuongeza ufanisi katika elimu kwa wasichana.
“Sio mtoto anapewa taulo siku mbili harafu hazionekani tena.Na kuna wengine wakipewa hizi zinaingia kwenye biashara,hilo ni kosa kubwa”alisema Ruth Msafiri
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminatha Mwenda,amesema wamefanikiwa kununua vifaa hivyo boksi 260 za taulo za kike zenye thamani ya zaidi ya milioni 9 kupitia mapato yao ya ndani na kukabidhi shule 24 kwa ajili ya wasichana 5636 waliopevuka ili kuwasitiri wanapokuwa hedhi.
“Tumenunua taulo za kike kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa wasichana ya kusoma vizuri,na katika bajeti yetu tumetenge Milioni 10 kwa ajili ya sekondari,na Milioni 10 kwa ajili ya shule za msingi.Leo tumewakabidhi sekondari”alisema Iluminatha Mwenda
Valeno Kitalika ni mkuu wa shule ya sekondari Joseph Mbeyela,kwa niaba ya wakuu wa shule wameishukuru serikali kwa msaada huo kwa ajili ya watoto kwa kuwa wataongeza ari ya kujisomea huku akitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitolea.
“Nimshukuru mkurugenzi na serikali ambao wameweza kutoa vifaa hivi kwa watoto,hawa watoto sasa wataongeza ari ya kusoma kwasababu ni vitu ambavyo vilikuwa vinawakwamisha kutokana na mahudhurio kuwa hafifu”alisema Valeno Kitalika
Elizabeth Mbigile ni mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya wasichana Josephine na Steria Muta ni kutoka shule ya Sekondari Maheve.Wameshukuru serikali kwa msaada huo huku wakiendelea kuwasaidi kwa kuwa shule zingine ziko mbali na maeneo ya huduma.
0 Comments