Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jamii mkoani Njombe na kwingineko hapa nchini
imetakiwa kuwa na moyo wa huruma kwa kuwasaidia watu wasio jiweza ili
kuhakikisha nao wanafuaraha kutokana na ukaribu unaojengwa katika jamii.
Wito umetolewa na Inspector Joel Mwakanyasa kutoka
jeshi la zima moto mkoani Njombe walipotembelea kituo cha watoto yatima cha Tumaini
Ilunda ili kujumuika nao katika kuunza vyema mwaka 2021 huku akitoa wito kwa
taasisi nyingine za kiserikali na binafsi kuona namna ya kugusa makundi
mbalimbali ndani ya jamii ambayo yanahitaji msaada.
“ tumepanga malengo yetu kila mwaka kwa ajili ya
kuwafariji watu wenye makundi maalum,tunaziasa taasisi zingine za kiserikali
kwasababu hii ni njia ya kutoa huduma kwenye jamii yetu”alisema Joel Mwakanyasa
Sister Magret Moyo ni mlezi wa kituo hiki ambaye
anakiri ujio wa wahisani katika kituo hicho umekuwa msaada mkubwa na unatia
faraja hasa kwa watoto yatima waishio katika kituo hicho ambao wengine
wamepoteza wazazi na wengine kuokotwa baada ya kutelekezwa na wazazi wao huku akiitaka
jamii kuacha tabia ya kutelekeza watoto.
“Kwanza tunashukuru kwa msaada ambao tumeupata na
tunatoa wito kwa jamii waendelee kuwatunza watoto vizuri badala ya kuwatupa na
kuwaweka kwenye mazingira hatarishi hasa vijana kwasababu wasichana wengi
wanapokuwa kwenye mazingira magumu basi wanachukua uamuzi wa kuwatelekeza
watoto”alisema Sister Magret Moyo
Jeshi la zimamoto mkoani Njombe limekuwa na utaratibu
wa kutembelea watu wanaohitaji msaada maalumu ili kuendelea kutoa huduma kwa
jamii ambapo zaidi ya mahitaji kama mafuta ya kupikia,juice,unga,mchele vyenye
thamani ya zaidi ya laki mbili vimekabidhiwa kwa kituo hicho.
0 Comments